Kituo Cha Fursa
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,vijana na Mahusioano kupitia Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa(FDC) inawatangazia wananchi(Vijana) wenye umri kati ya miaka 15 na 35 fursa ya kujiungana mafunzo ya ufundi. Serikali itafadhili ada ya Mafunzo kwa 100%. Mwanafunzi/Mzazi/Mlezi atagharamia nauli ya kwenda na kurudi chuoni muda wote wa mafunzo.Muda wa Mafunzo ni miezi 6 na miezi 2 ni ya vitendo yaani jumla miezi nane 8. Katika fani za Ufundi umeme wa Majumbani,Ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo,Upishi,Kilimo,Mifugo,Ufundi wa Magari. Wasiliana nasi kwa namba +255 764 784 770(Mkuu wa Chuo),+255 713 423 475(Mratibu Mafunzo),+255 741 234 234(Maulizo) au tembelea ofisi zetu zilizopo Bigwa,Morogoro. Fomu zinapatikana Chuoni(Bure),mwisho wa kurudisha fomu ni 19 Disemba 2025 na Mafunzo yanaanza 26 Januari 2026.