Kituo Cha Fursa
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa kipo Mkoa wa Morogoro katika Manispaa ya Morogoro Mjini kilometa nane (8) kutoka Morogoro Mjini kipo Kata ya Bigwa. Chuo kinatoa fani mbali mbali za Muda mrefu (long-term) hadi miaka mitatu katika ngazi ya kwanza hadi ya tatu (NVA Level I,II & II), Kozi za Mudamfupi katika Mapishi na Lishe,Ushonaji na Tehama na Mafunzo maalumu (Tilor Made courses),na elimu ya sekondari (Programu ya Elimu Haina Mwisho (EHM)) kwa wasichana walioshindwa kuhitimu elimu ya sekondari katika mfumo rasmi kwa sababu mbali mbali.
Sifa za kujiunga na Chuo ni kwa mtanazania yoyote mwenye umri wa miaka 17 na kuendelea mwenye uwezo wa kusoma na kuandika vizuri.