Kituo Cha Fursa
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa leo tarehe 21 Nov 2025 kimeadhimisha mahafali yake ya kumi na saba kwa wanafunzi wa ngazi ya pili katika fani mbalimbali za ufundi,ikiwemo Ufundi umeme,Magari,Uashi,Mapishi na lishe,Ushonaji,Kilimo,na Mifugo. sherehe hiyo imefanyika katika viwanja vya chuo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo viongozi wa serikali,wanakijiji,wazazi,na walimu/Wakufunzi.