Coat of Arms

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa

“ Kituo Cha Fursa ”

KSW Logo

CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI BIGWA CHASHEREHEKEA MAHAFALI YA 25

📅 October 6, 2026
CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI BIGWA CHASHEREHEKEA MAHAFALI YA 25
MAHAFALI YA 25 – BIGWA FDC 2026
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa kimefanya Mahafali ya 25 ya mwaka 2026, yakihudhuriwa na wahitimu kutoka programu mbalimbali za mafunzo ya ufundi na ujuzi zinazotolewa chuoni.

Mahafali hayo yamewakutanisha wahitimu wa fani mbalimbali, zikiwemo Ufundi Umeme wa Majumbani, Ufundi Magari, Ubunifu wa Mavazi na Ushonaji Nguo, Upishi, Ufugaji na Kilimo.

Aidha, katika mahafali hayo, wanagenzi 137 waliopata mafunzo ya kozi fupi kwa ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, wamehitimisha mafunzo yao. Wanagenzi hao walianza mafunzo tarehe 19 Januari 2026 na kuyakamilisha tarehe 18 Septemba 2026.

Sambamba na hilo, wanachuo 97 wa programu za mafunzo ya muda mrefu kwa mwaka wa masomo 2025/2026 wamehitimu mafunzo yao katika fani mbalimbali.

Mahafali haya yanaendelea kuonesha mchango wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa katika kuwawezesha vijana na wanajamii kupata ujuzi, maarifa na stadi za kazi zinazoweza kuwawezesha kujiajiri, kuajiriwa na kuchangia maendeleo ya jamii.

Hongera kwa wahitimu wote wa Mahafali ya 25 ya Bigwa FDC!

Takwimu

8 Fani zinazotolewa
25 Watumishi
380+ Wanafunzi
10,000+ Wahitimu